Life Ya Ghetto

LIFE YA GHETTO
Spoken Word Poem

Kevo Ule Wa Mistari

Nyumba zimeinama,
Maisha ni lawama,
Kazi hakuna na bado tunang’ang’ana,
Ex amenikana,
Usanii nafanya na bado sijajulikana,
Maisha imekua ngumu,
Natamani kunywa sumu,

Nahustle daily nipate ata za kulipa keja,
Na Boss nikimpigia, simu yake ni mteja,

Madeni nimejaza ata kwa mama kibanda,
Na lala chini siezi afford ata kitanda,
Irony ni kua, imagine naitwa Gitonga?
Nadream yangu ni ati one day nitakaa kwa bedsitter,
Even though sai sijalipa rent ya miezi sita,

Juzi baby mama alinidai doh ya kupeleka mtoto shule,
Nikamshow zih it’s too late,
Itabidi umenipenda bure,

Alijaribu ku-insist akanishow angalaa nipe doh ya salon,
Nikamshow zih ata leo naona ukikula kwa mama yako,

The truth is sina na siwezi iba ndo nipate,
Kiamsha kinywa si lazima ikue na mkate,
The truth is me hulala ata nikiwa kinenge,
No wonder siezi mind ata nikipewa malenge,
The truth is ata nikimeditate na mambichwa,
Bado nitawaza bongo nikikuna kichwa,

Nimeona mayouth Ghetto wakizama,
Hata Gava imetuekea lawama,
Nimeona watoi wakipata mimba,
Nama baby daddy wakiambiwa wanadinda,

At Sixteen si Kim alikua mzazi?
At Seventeen si alipigwa risasi?

Sina kitu mfukoni na dryspell imeniweza,
Niko na appetite na mate ndo nameza,
Life imenigonga Ten-Nil sai nko chini ya meza,
Na madander tulisoma nawao sai wameweza,

Jah Jah ree mbona life umenigeuzia?
Si daily kwa prayer bado naulizia?
Si ulisema binadamu tuwe kind?
Lakini cheki wananionea wivu hata wale blind

Lakini yote yakisemwa,
Chuki ni kama kikohozi na itatemwa,
Najua everything happens for a reason,
No wonder umenikeep away from prison

©Mistari Productions

Published by Stylishkay

Am a Poetry enthusiast.

Leave a comment

Design a site like this with WordPress.com
Get started